Thursday, December 20, 2012

Mnyika amkomalia Mwakamele


MBUNGE wa Ubungo, John Mnyika amemshukia mmiliki wa Kampuni ya McDonald Live Line, kuhusu ufisadi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), akimtaka kujibu hoja za msingi zinazomhusu.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mnyika (picha ndogo chini) alisema mmiliki huyo, Donald Mwakamele, hayajibu hoja zilizomo katika orodha ya kwanza ya watuhumiwa wa ufisadi na uzembe katika Tanesco, aliyoitoa kuhusu mikataba ya kampuni yake ya McDonald Live Line Technology Limited.
Hali kadhalika kampuni nyingine ya Santa Clara Supplies Ltd kuhusu masuala yaliyofanyika kinyume cha sheria.
“Kauli ya Mwakamele kwamba yupo kiongozi mmoja wa Tanesco ambaye alimwomba rushwa ya Sh100 milioni, ikiwa ina ukweli inazidi kudhihirisha kuwa mtandao wa ufisadi ulioko ndani ya Tanesco na Mwakamele, anapaswa kuhojiwa na Takukuru, ili ataje jina la mtuhimiwa huyo wa ufisadi,” alisema Mnyika.
Alisema mfanyabiashara huyo anapaswa kutioa sababu za kuficha jina na mtuhumiwa wa ufisadi huo.
Mnyika alisema badala ya Mwakamele kumlipa Sh20 milioni, ili azitumie kwenda mahakamani kama anaamini kwamba vielelezo havipo kuhusu maelezo aliyoyatoa katika orodha ya watuhumiwa wa ufisadi na uzembe katika Tanesco, anapaswa kujibu hoja.
“Katika hatua ya sasa ajitokeze hadharani na kujibu hoja za msingi zilizoko katika orodha hiyo,” alisema Mnyika.
Alisema majibu ya Mwakamele na ukimya wa Bodi ya Tanesco kuhusu orodha ya watuhumiwa, unathibitisha haja ya mamlaka nyingine za kiserikali, kuchukua hatua.
Mamlaka hizo ni pamoja na Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai, Mkurugenzi wa Mashtaka, Mamlaka ya Ununuzi wa Umma (PPRA), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Sekretariati ya Maadili ya Umma.

Monday, December 17, 2012

KARIBU KATIKA BLOG YAKO

Karibu tusome na tujifunze mambo kibao yanayotokea kila pembe ya nchi yetu. hii nikila siku tunapata ishu mpya ambayo inakupa mwanzo wa siku yakoo.